MVUA YASIMAMISHA MECHI ZA US OPEN
Michuano ya US Open
kwa upande wa kinadada imesimamishwa kwa muda baada ya mvua kali
kunyesha hali iliyosababisha ugumu wa mchezo huo. Serena Williams
atapaswa kusubiri mpaka ijumaa ya leo kuendelea na ratiba ya kalenda ya
Grand slam ya nusu fainali kwa wanawake ambapo atacheza dhidi ya Roberta
Vinci.
Hali hiyo ya mvua haikuzuia mchezo wa wanaume na uliendelea kama
ulivyopangwa ambapo matumaini ya bara la Afrika kuendelea kuwepo katika
michuano hiyo yalifikia tamati baada ya Kevin Anderson wa Afrika Kusini
kushindwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa na
Stan Wawrinka seti 6-4 6-4 6-0.
Hivyo kwa wanaume nusu fainali itakuwa:
Roger Federer vs Stan Wawrinka.
Novak Djokovic vs Marin Cilic.
No comments:
Post a Comment