Saturday, 11 February 2017

JUMAMOSI KUFUNGUKA KWA ARSENAL-HULL, WENGER AUNGAMA ‘WAKO NJIA PANDA!’


WENGER-WIMARatiba
Jumamosi Februari 11
1530 Arsenal v Hull City             
1800 Manchester United v Watford                 
1800 Middlesbrough v Everton    
1800 Stoke City v Crystal Palace           
1800 Sunderland v Southampton
1800 West Ham United v West Bromwich Albion                 
2030 Liverpool v Tottenham Hotspur     
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
BAADA vipigo viwili mfululizo mikononi mwa Chelsea na Watford, Arsenal Jumamosi wako kwao Emirates kucheza Mechi ya EPL, Ligi Kuu England na Hull City ambao Majuzi waliitwanga Liverpool 2-0.
Mechi hiyo ya Arsenal na Hull City ndio ya kwanza kabisa kwa hiyo Jumamosi na kufuatiwa na Mechi nyingine 6 za EPL ambapo Jioni huko Ols Trafford Manchester United wataikaribisha Watford na Usiku kimbembe kiko Anfield kati ya Timu ya 5 ya EPL Liverpool ikiikaribisha Timu ya Pili Tottenham Hotspur.
Kufuatia vipigo hivyo viwili Arsenal imeteleza hadi Nafasi ya 4 kwenye EPL wakiwa Pointi 12 nyuma ya Vinara Chelsea na kuifanya Mechi hiyo na Hull City kuwa muhimu mno kwa EPL-FEB5Arsenal.
Lakini pia Wiki ijayo, Arsenal wanasafiri kwenda Germany kucheza na Vigogo wa huko Bayern Munich kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kisha Arsenal wako Ugenini tena kucheza na Timu isiyo kwenye Ligi rasmi huko England, Sutton United ikiwa ni Mechi ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP.
Mechi hizi zimemfanya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger aungame kuwa zitaamua Msimu wao kwa vile wako njia panda kufuatia vipigo mfululizo.
Amesema: “Tunatoka kwenye matokeo ya kuvunja moyo. Ni wakati mgumu na wa changamoto kubwa. Tunacheza na Hull Nyumbani kisha Championz Ligi na badae FA CUP. Jinsi tutakavyokabili Mechi hizi zitaamua Msimu wetu!”
EPL – Ligi Kuu England
Ratiba
Jumapili Februari 12
1600 Burnley v Chelsea    
1900 Swansea City v Leicester City                 
Jumatatu Februari 13
2300 Bournemouth v Manchester City

No comments:

Post a Comment