Tuesday, 1 March 2016

WAGOMBEA WASUBIRI JUMANNE KUU MAREKANI


MajimboImage copyrightAP
Image captionMajimbo 12 yanafanya uchaguzi wa mchujo leo
Wagombea wanaowania kupeperusha bendera za vyama vya Republican na Democratic katika uchaguzi wa urais Marekani wanajiandaa kwa siku muhimu sana uchaguzi wa mchujo, siku ya Jumanne Kuu.
Majimbo 12 yatafanya mchujo siku ya leo kwenye kinyang’anyiro ambacho kitaamua hatima ya wagombea.
Majimbo hayo ni kuanzia Massachusetts mashariki hadi Alaska kaskazini magharibi.
Baada ya mchujo kufanyika katika majimbo manne, Donald Trump anaongoza upande wa Republican naye Hillary Clinton upande wa Democratic.
SenataTed Cruz anahitaji kumshinda Bw Trump jimbo Texas, jimbo lake la nyumbani.
USImage copyright
Image captionKutoka kushoto: Marco Rubio, Donald Trump na Ted Cruz
Bw Trump naye anahitaji sana kushinda Massachusetts, jimbo lenye wapiga kura wengi wa msimamo wa kadiri.
Bi Clinton anatumai ataweza kuendeleza ushindi wake, baada ya kushinda jimbo la South Carolina wikendi. Katika jimbo hilo, alipata kura nyingi kutoka kwa Wamarekani weusi baada ya kushindwa mchujo uliotangulia jimbo la New Hampshire na mpinzani wake mkuu Bernie Sanders.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika tarehe 8 Novemba kumchagua mrithi wa Rais Barack Obama ambaye ni wa chama cha Democratic.
Chini ya uongozi wa Rais Obama, chama cha Republican kimefanikiwa kutwaa udhibiti wa mabunge yote mawili ya Congress.
Bw Trump anaongoza katika kura za maoni katika majimbo yote 11 ya chama cha Republican yatakayofanya mchujo Jumanne.
Majimbo hayo ni Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia, Alaska na Minnesota.

No comments:

Post a Comment