MAN UTD KUMKOSA ROONEY MECHI YA UEFA
Mshambuliaji wa
Manchester United Wayne Rooney ameachwa nje ya kikosi kitakachocheza
mechi ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya Jumanne ugenini PSV Eindhoven kwa
sababu ya jeraha.
Rooney, 29, hakucheza kwenye mechi yao dhidi ya
Liverpool Jumamosi baada yake kuumia misuli ya paja akifanya mazoezi.
Kilabu hiyo ya Old Trafford ilishinda 3-1 kwenye mechi hiyo.
Mkufunzi
mkuu wa Red Devils Louis van Gaal alisema kulikuwa na shaka kuhusu
mchezaji huyo baada ya mechi hiyo, na sasa amesema ameamua
kutobahatisha.
Mshambuliaji James Wilson na kiungo wa kati Andreas Pereira wamejumuishwa kikosini.
Wawili
hao hawajacheza mechi yoyote msimu huu, na majuzi Wilson alihusishwa na
kuhamia kilabu inayocheza ligi ya daraja la pili kwa mkopo.
Pereira naye amechezea klabu hiyo mechi mbili pekee akiingia kama nguvu mpya, tangu ajiunge nao kutoka PSV Agosti mwaka jana.
Mechi
hiyo ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya itakayochezwa Jumanne uwanja wa
Phillips itakuwa ya kwanza kwa Manchester United kwenye kampeni yao
Kundi B.
No comments:
Post a Comment