UPINZANI WAITISHA MAANDAMANO DRC
Vyama kadhaa vya
upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vimeitisha maandamano
katika mji mkuu wa taifa hilo Kinsasha dhidi ya kuahirishwa kwa uchaguzi
wa urais uliotarajiwa mwezi Novemba mwaka 2016.
Wiki iliopita
,mahakama ya kikatiba nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo
kuangaziwa upya ,hatua ambayo wapinzani wanasema ni ya kutaka rais
Joseph Kabila kusalia mamlakani zaidi hata baada ya kukamilika kwa muda
wake uliowekwa kikatiba.
Mabango yaliobebwa na vyama hivyo yalisoma ''mabadiliko ya uongozi ni sharti yafanyike''.
Maandamano ya kupinga kucheleweshwa kwa uchaguzi huo
yalizua ghasia mnamo mwezi Januari na kusababisha vifo vya takriban
watu 36.
Bwana Kabila amekuwa madarakani tangu babaake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka 2001.
No comments:
Post a Comment