JESHI LA MISRI LADAI KUUA KIMAKOSA
Misri imesema jeshi
lake la ulinzi limeua raia 12 kwa bahati mbaya,wakiwemo watalii kutoka
Mexico wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imetuma kikosi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Kwa
upande wa Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amekemea tukio hilo na
kusema kuwa ameitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi wa kina, Wizara
ya mambo ya nje ya Mexico imethibitisha kuwa takriban raia wake wawili
wameuawa na kuongeza kuwa inafanya jitihada kuwatambua waathirika
wengine.
Tamko la wizara limesema , Balozi wa Mexico nchini Misri, Jorge Alvarez Fuentes alitembelea hospitali na kuzungumza na raia watano wa Mexico ambao hali zao zilikuwa njema.
No comments:
Post a Comment