AZAM TV SASA RASMI WAZINDUA LA LIGA, WATU KUSHUHUDIA MECHI LIVE MWANAONE
Runinga ya Azam TV leo rasmi imezindua uonyeshwaji wa Ligi maarufu ya Hispania ya La Liga.
Uzinduzi huo umefanyika makao makuu ya Azam TV, Tabata jijini Dar es Salaam na wageni kadhaa walialikwa.
Kupitia ving’amuzi vya Azam TV, sasa watu wataweza kuona mechi mbalimbali za La Liga wakianza na ile ya Ijumaa ijayo kati ya Malaga dhidi ya Sevilla.
Azam TV inakuwa kampuni ya kwanza ya Tanzania inayomiliki runinga kupewa haki ya kuonyesha mechi za La Liga ambayo ni ligi yenye mafanikio makubwa zaidi katika kipindi hiki.
...TORRINGTON AKIFANYA YAKE. |
TIDO MHANDO AKIFAFANUA JAMBO... |
SEHEMU YA WAGENI WAALIKWA, SHAFFIH DAUDA, SAID TULLY NA EDO KUMWEMBE WALIKUWEPO. |
FLORIAN KAIJAGE ALIYEKUWA MWENDESHA SHUGHULI PIA ALIKUWEPO |
No comments:
Post a Comment