WENYEJI Chile wameanza vyema michuano ya mataifa ya America kusini baada ya usiku wa kuamkia leo kuichakaza Ecuador magoli 2-0 katika mechi ya ufunguzi ya kundi A.
Siku kadhaa baada ya kukosa taji la Uefa Champions League akiichezea timu yake ya Juventus ambapo walifungwa 3-1 na Barcelona katika mechi ya fainali, Arturo Vidal ameanza vizuri Copa America kwani ndiye aliyeifungia Chile goli la kwanza dakika ya 67′ kwa mkwaju wa penalti.
Bao la pili la Chile lilitiwa kimiani na Eduardo Vargasa katika dakika ya 84′
No comments:
Post a Comment